Huwezi kusikiliza tena

Vijana waliozaliwa na Ukimwi wajieleza

Ikiwa ulimwengu leo unaadhimisha siku ya UKIMWI duniani, idadi vijana wadogo wanaokufa kwa UKIMWI imeongezeka mara tatu katika miaka 15 iliyopita.

Ripoti ya shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto UNICEF iliyotolewa hivi karibuni inasema UKIMWI unaongoza kwa kuua vijana wengi wadogo barani Afrika na wa pili kwa kuua vijana hao duniani kote.

Kwa mujibu wa ripoti hiyo wengi wanaokufa kwa hivi sasa ni wale waliozaliwa na virusi takribani miaka 15 iliyopita wakati ambapo mama zao walikuwa hawana mwamko wa kutumia dawa za kukinga maambukizi toka kwa mama kwenda kwa mtoto.

Mwandishi wetu wa Nairobi Muliro Telewa alitembelea Magharibi mwa Kenya ambako alikutana na vijana waliojitangaza kuzaliwa wakiwa na maambukizi ambapo wanaeleza baadhi ya changamoto walizo nazo…