Huwezi kusikiliza tena

Je wajua unaweza pata mkaa kutokana na kinyesi ?

Mji mkuu wa Ghana Accra umetajwa kama moja ya miji iliyochafuliwa zaidi duniani.

Hii ni kwa mujibu wa takwimu zilizodhihirisha kuwa uchafu wa jiji hilo hutupwa katika maeneo ya makazi duni katika vitongoji vyake.

Hali hii inatokana na kutokuwepo kwa muundo msingi dhabiti wa kutoa maji taka.

Wenyeji wanaokisiwa kuwa takriban watu milioni 4 wanategemea malori ya kufyonza yabisi na maji taka kwa huduma hiyo.

Wenye malori hayo nao wanamwaga maji taka baharini kwa sababu ya ukosefu wa sheria zinazodhibiti utupwaji wa maji hayo.

Huku maelfu ya wajumbe wakiendelea kujadili mabadiliko ya tabia nchi ,takriban kilomita 6,500 kutoka huko kundi moja la vijana limechukua jukumu la kupunguza madhara ya uchafuzi wa maji ya bahari kwa kutengeneza mkaa kutokana na yabisi inayotenganisha na maji taka.

Wameiambia BBC kuwa wanakusudia kuiga mradi huo kote nchini.