Nyangalio
Huwezi kusikiliza tena

Fundi wa nguo asiyeona aliye maarufu sana Tanzania

Katika maadhimisho ya siku ya walemavu duniani, tulikutana na bwana Abdallah Nyangalio. Yeye ana umri wa miaka 56 ana watoto wanane.

Kabla ya kupoteza uwezo wake wa kuona alikuwa anauza nguo kuukuu mjini Daresalaam.

Lakini umaaarufu zaidi amepata baadaye ambapo kazi aliyoanza ya kushona nguo licha ya kutoona imemkutanisha na watu maarufu akiwemo aliyekuwa rais Jakaya Kikwete na mke wa rais wa zamani Anne Mkapa.

Sammy Awami amezungumza naye mjini Daresalaam.