Rwanda
Huwezi kusikiliza tena

Sodo za mabaki ya migomba Rwanda

Mradi wa kipekee umeanzishwa nchini Rwanda wa kutengeneza sodo ama taulo zinazotumiwa na wanawake wakati wa hedhi kwa kutumia nyuzi zitokanazo na mabaki ya migomba.

Lengo ya mradi huu ni kupunguza idadi kubwa ya watoto wa kike wanaoshindwa kwenda shule wakati wakiwa mwezini kwa kukosa pesa za kununua sodo.

Mwandishi wa BBC Yves Bucyana alitembelea mradi huo mashariki mwa Rwanda na kutuandalia taarifa ifuatayo.