Treni yarejealea huduma zake mjini Kampala
Huwezi kusikiliza tena

Huduma ya treni yarejea Kampala

Kwa mara ya mwisho abiria wa treni kutumia stesheni ya Kampala ilikuwa mwaka 1998. Leo basi, huduma ya treni imerejea tena kwenye stesheni hiyo ya Kampala, na watu wamefurahia. Usafiri wa abiria utakuwa wa umbali wa kilomita 14 kati ya mjini Kampala na viunga vya mji huu upande wa mashariki. Mwandishi wetu Siraj Kalyango anasimulia zaidi kutoka Kampala.