Huwezi kusikiliza tena

Wakulima Afrika kufaidika?

Mataifa ya Afrika yanayohudhuria kongamano la shirika biashara duniani jijini Nairobi WTO wameshinikiza wiki nzima kupata usawa wa biashara kwenye soko la kimataifa.

Wanahisi kuwa ruzuku wanayopewa wakulima kwenye mataifa yaliyoendelea inawezesha kuuza bidhaa kwa bei ya chini na kuwaumiza wakulima wa nchi masikini wasio na ruzuku.

Mwandishi wetu Ferdinand Omondi ametembelea shamba la maua katika eneo la Bonde la Ufa nchini Kenya ili kuelewa zaidi biashara ya kimataifa.