Mitaa ya Bujumbura
Huwezi kusikiliza tena

Amani ya Burundi bado haijatengamaa

Hali imezidi kuwa ya wasi wasi nchini Burundi kufuatia Watu watatu kujeruhiwa mjini Bujumbura baada ya mabomu matatu kurushwa hadi eneo lililo karibu na afisi ya meya kati kati mwa mji mkuu.

Burundi imekumbwa na machafuko tangu Rais Pierre Nkurunziza kutangaza kuwania mhula wa tatu na kufanikiwa kuchukua hatama za uongozi wa nchi hiyo.

Taharuki imeanza kutanda tena Bujumbura baada ya siku chache za utulivu.mwandishi wa BBC, Regina Mziwanda amezungumza na mwandi wa BBC mjini Bujumbura Kibuga Ramadhani kutaka kujua baada ya tukio hilo hali ikoje ya usalama kwa sasa.