Kichina
Huwezi kusikiliza tena

Kichina kufundishwa shuleni Tanzania

Tanzania inatarajia kuanza kufundisha lugha ya Kichina kama somo katika shule za sekondari hasa kidato cha tano na cha sita. Tayari Wataalamu wa lugha hiyo kutoka China wamekuja nchini Tanzania kusaidia katika kutengeneza na kuanzisha mtaala wa lugha hiyo.

Serikali imetenga shule zipatazo sita ambazo mradi wa majaribio ya ufundishwaji wa lugha hiyo utafanyika, ikiwa ni shule kutoka mkoa wa Dodoma, Morogoro na Dar es Salaam.

Mwandishi wa BBC Sammy Awami alizungumza na Kaimu Mkurugenzi Idara ya Ithibati Bi Khadija Mcheka kuhusu hili.