Shamsa
Huwezi kusikiliza tena

'Tunafurahia sana kurudi chuoni Garissa'

Shamsa Abdi Barre ni mmoja wa wanafunzi waliorejea katika Chuo Kikuu cha Garissa kuendelea na masomo baada ya chuo hicho kufunguliwa tena.

Yeye ni mwanafunzi wa mwaka wa tatu. Chuo hicho kilifungwa baada ya wanamgambo wa al-Shabab kushambulia na kuua watu 148.

Amezungumza na mwandishi wa BBC Bashkas Jugsodaay.