Maalim
Huwezi kusikiliza tena

CUF yapinga marudio ya uchaguzi Zanzibar

Chama cha CUF nchini Tanzania kimeshikilia msimamo wake kwamba marudio ya uchaguzi visiwani Zanzibar si suluhisho la mgogoro wa kisiasa unaoendelea visiwani humo.

Na kwamba zaidi, marudio hayo yatasababisha vurugu. Kauli hii imetolewa na Katibu Mkuu wa chama hicho Maalim Seif Shariff Hamad jijini Dar es Salaam leo asubuhi baada ya mfululizo wa vikao ambavyo vyama vya CUF na CCM vimekuwa vikivifanya kwa takribani miezi mitatu sasa tangu mgogoro wa kisiasa uibuke baada ya kufutwa kwa uchaguzi mwezi Oktoba mwaka jana.

Mwandishi wa BBC Sammy Awami amezungumza na Maalim Seif Sharif Hamad.