Wanamitindo
Huwezi kusikiliza tena

Fani ambayo wanawake huwazidi wanaume

Ni kawaida kusikia watu wakitaka mishahara isawazishwe kwa jinsia zote, lakini sana ni wanawake wanaolipwa mishahara ya chini kuliko wanaume.

Lakini hali ni tofauti katika fani ya mitindo Uingereza, ambapo wanamitindo wa kike hulipwa zaidi ya maradufu mshahara wanaolipwa wenzao wa kiume, kwenye maonyesho ya mitindo na katika picha za kuchapishwa kwenye majarida.