Huwezi kusikiliza tena

Jimbo la Anglikana Marekani lasimamishwa

Kanisa la Kianglikana duniani limelisimamisha jimbo kuu la kanisa hilo nchini Marekani kushiriki taratibu za kanisa hilo kama adhabu.

Adhabu hiyo imetolewa kutokana na kanisa hilo, kutambua ndoa za watu wa jinsia moja kinyume na mafunzo ya biblia.

Mkutano wa maaskofu wakuu wa kanisa hilo huko Canterbury Uingereza umetoa kauli kwamba ndoa ni kati ya mwanamme na mwanamke, na kwamba kanisa Anglikana nchini Marekani limeondokana na imani inayozingatiwa na Waanglikana walio wengi.

Halima Nyanza amezungumza na Peter Musembi wa BBC, na kutaka ufafanuzi kidogo juu ya kauli hii ya kanisa Anglikana.