Fadhumo
Huwezi kusikiliza tena

Mwanamke anayetaka kuwa rais Somalia

Anataka kuwa mwanamke wa kwanza kuiongoza Somalia kama rais wa nchi hiyo, lakini je atachaguliwa? Kutana na Fadhumo Dayib mwenye umri wa miaka 44.

Ni mama wa watoto wanne, na tangu atangaze nia ya kuwania kiti hicho amekabiliwa na vitisho vya kuuawa, lakini anasema hakuna kitu kitakacho mzuia katika azma yake ya kuwa rais wa nchi hiyo.

Uchaguzi utafanyika mnamo mwezi Septemba mwakani.

Amezungumza na mwandishi wa BBC Ruth Nesoba.