utalii kenya
Huwezi kusikiliza tena

Sekta ya utalii yaanza kuimarika Kenya

Sekta ya utalii nchini Kenya imeanza kuonyesha dalili za kuimarika tena baada ya karibu miaka mitatu ikiwa katika hali mbaya. Hofu za mashambulio ya kigaidi ziliwafanya watalii kuepuka hoteli za nchi hiyo, huku sekta ikipoteza mamilioni ya dola, na zaidi ya watu elfu thelathini kupoteza kazi zao. Mwandishi wetu Ferdinand Omondi anaripoti akiwa Ukunda, kusini mwa pwani ya Kenya.