Meli ya maktaba Mv Logos
Huwezi kusikiliza tena

Maktaba inayoelea yazuru Dar es Salaam Tanzania

Maktaba kubwa zaidi inayoelea, MV Logos Hope imefanya safari yake ya kwanza Dar es salaam, Tanzania. Meli hiyo imekuwa ikisafiri kwa muda wa miaka minne, ikiwa na madhumuni ya kuhamasisha utamaduni wa kusoma vitabu hasa kwa vijana. Mwandishi wetu Tulanana Bohela amehudhuria ufunguzi wa maonyesho ya vitabu na kututumia taarifa hii.