Zika
Huwezi kusikiliza tena

Virusi vya Zika viligunduliwa Uganda

Virusi vya zika vinasambaa kwa kasi, kwa mujibu wa ripoti kutoka shirika la afya duniani WHO, ambalo limeunda kamati ya dharura kukabiliana na virusi hivyo.

Nchi 20 kote duniani zimekutwa na virusi hivyo hususan Amerika ya Kusini. Virusi hivyo vinasambazwa na mbu, na vinasababisha watoto kuzaliwa na ulemavu uitwao - micro-cephaly.

Virusi hivyo vimewahi kugundulika Afrika na Asia lakini mwanzo viligunduliwa Uganda.

Siraj Kalyango amefuatilia utafiti wa virusi hivyo huko Uganda.