Huwezi kusikiliza tena

Mabunge yaliyoshuhudia vurugu duniani

Wabunge wa chama cha Economic Freedom Fighters (EFF) chake Julius Malema walifurushwa bungeni Afrika Kusini baada ya kuzua fujo wakati wa hotuba ya Rais Jacob Zuma.

Wanamtaka aondoke madarakani kutokana na tuhuma za utumizi mbaya wa pesa za umma ambazo zinamkabili. Visa vya wabunge kuzua fujo bungeni vimetokea katika mabunge kadha duniani.

Nchini Ukraine, Desemba mwaka jana Waziri Mkuu Arseniy Yatsenyuk aliinuliwa juu juu alipokuwa akitoa hotuba. Nchini Kosovo mwezi Septemba, wabunge wa upinzani walimrushia mayai Waziri Mkuu Isa Mustafa.

Japan, Nepal na Kenya visa sawa vimeshuhudiwa.