Museveni
Huwezi kusikiliza tena

Museveni: Uchaguzi Uganda ulikuwa shwari

Rais wa Uganda Yoweri Museveni ambaye ameshinda uchaguzi uliofanyika wiki iliyopita amekanusha madai ya upinzani ya kuwepo wizi wa kura na pia kupuuza shutuma za waangalizi wa kimataifa.

Amezungumza na mwandishi wa BBC Zuhura Yunus katika mahojiano maalum Nyumbani kwake Rwakitura Magharibi mwa Uganda Museveni akianza kwa kuzungumzia kuzuiliwa Nyumbani kwa mpinzani wake Dkt Kizza Besigye.