Zanzibar
Huwezi kusikiliza tena

CUF: Hatutambui uchaguzi wa marudio Zanzibar

Tume ya Uchaguzi ya Zanzibar (ZEC) kupitia Mwenyekiti wake, Jecha Salum Jecha, mwanzoni mwa juma hili ilitangaza kuwa hakuna chama wala mgombea hata mmoja aliyefuata masharti yanayotakiwa kuweza kujitoa kwenye uchaguzi wa marudio unaotazamiwa kufanyika tarehe 20 Machi visiwani humo na hivyo wote ni wagombea halali.

Chama kikuu cha Upinzani visiwani humo CUF kupitia mahojiano na mwandishi wa BBC Arnold Kayanda na Kaimu Mkurugenzi Habari na Mawasiliano ya Umma, Hamad Masoud Hamad, kimesema msimamo ni ule ule, hata kikishinda uchaguzi wa marudio, hawatautambua uchaguzi wa marudio.