Katumbi
Huwezi kusikiliza tena

Moise Katumbi anaweza kuwa rais DR Congo?

Rais wa klabu maarufu katika Jamhuri ya kidemokrasia ya Congo TP Mazembe, Bw Moise Katumbi sasa anataka kuwa rais wa nchi hiyo kubwa ya Afrika ya kati.

Bwanyenye huyo maarufu, ni mgombea wa urais katika uchaguzi mkuu unaoratibiwa kufanyika mwezi Novemba mwaka huu.

Katumbi ambaye amewahi kuwa gavana wa jimbo tajiri zaidi nchini humo la Katanga alijiuzulu na kuwa mpinzani mkuu wa Rais Joseph Kabila.