Said
Huwezi kusikiliza tena

Mbona AFP wanashiriki uchaguzi Zanzibar?

Pamoja na kwamba Chama cha Upinzani cha CUF kinachoongozwa na Makamu wa kwanza wa Rais visiwani humo kimesusia kushiriki uchaguzi huo wa marudio kwa madai kuwa kilishinda Uchaguzi wa awali, vyama vingine vya upinzani vimesalia katika kinyang'anyiro hicho kwa lengo la kuking'oa madarakani Chama cha Mapinduzi CCM.

Arnold Kayanda aliyeko Mkoa wa Kusini Magharibi, Wilaya ya Chake Chake Kisiwani Pemba amezungumza na Mgombea Urais kupitia Chama cha Alliance of Farmers Party AFP, Said Soud Said kwanza akitaka kujua mbona wao wameenda Kinyume na wapinzani wenzao?