Mose fan fan
Huwezi kusikiliza tena

Mwanamuziki Mose ''fan fan'' kutumbuiza mashabiki Kenya

Mwanamuziki maarufu wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, Mose Fan Fan, yuko Kenya kwa hivi sasa kutumbuiza mashabiki wa muziki wa rhumba na bendi yake ya Somo Somo. Fan Fan, kwa jina lake kamili Mose Se Sengo, ana umri wa miaka 70 na makao yake ni London. Miongoni mwa wanamuziki wa DRC aliocheza nao ni marehemu Luambo Luanzo Makiadi, gwiji wa rhumba nchini humo. Mose Fan Fan amealikwa na mwanariadha mashuhuri wa zamani wa Kenya Rose Tata Muya

John Nene amezungumza na 'Fan Fan' na kumuuliza zaidi kuhusu wimbo wake ambao unavuma sana nchini Kenya kwa sasa, Papa Lolo