Sanders
Huwezi kusikiliza tena

Ndege aingilia mkutano wa Bernie Sanders

Mgombea urais wa chama cha Democratic nchini Marekani Bernie Sanders alikatiza hotuba yake kwa muda baada ya ndege kutua kwenye jukwaa akihutubia mkutano wa kampeni.

Umati uliohudhuria mkutano huo katika mji wa Portland, Oregon ulishangilia.

Sanders, anayeshindana na Hillary Clinton, alishinda majimbo matatu yaliyofanya mchujo Jumamosi.

Majimbo hayo ni Washington, Alaska na Hawaii.