Huwezi kusikiliza tena

Mvutano juu ya Mradi wa Bomba la Mafuta

Serikali ya Tanzania na Kenya ziko kwenye mazungumzo juu ya mvutano uliopo kuhusu mradi wa Bomba la mafuta kutoka Uganda.

Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini wa tanzania Profesa Justin Ntalikwa amesema nchi hizo mbili zinakutana kumaliza mvutano huo.

Sikiliza ripoti ya Noel Mwakalindile juu ya hilo pamoja na kuhusiana na mkutano kati ya Wizara ya Nishati na Madini na wafanyabiashara wa sekta ya Mafuta uliolenga kutazama fursa za mradi huo wa bomba la mafuta kutoka Uganda mpaka katika bandari ya Tanga Tanzania.