Nywele
Huwezi kusikiliza tena

Nywele bandia zilizo ghali kama gari

The Salon ni msururu wa mazungumzo na wanawake kutoka maeneo mbalimbali duniani kuhusu utambulisho na muonekano, katika kiti cha kusukwa nywele.

Jijini Johannesburg, Afrika Kusini, Tracy hatimaye anasukwa kwa kutumia nywele bandia ghali kutoka “Brazil” ambazo mamake Hope amefanikiwa kumnunulia kwa kuzilipia kidogo kidogo kila mwezi. Gharama ya jumla ya mtindo huo wa nywele ni kama “kununua sehemu ya gari lakini anaivalia kichwani,” anasema Hope.