Uber
Huwezi kusikiliza tena

Upinzani dhidi ya Uber waendelea Kenya

Kampuni ya kimataifa ya magari ya teksi, Uber, inaendelea kuimarika barani Afrika, huku ikiwavutia wateja kwa sababu ya nauli nafuu.

Lakini katika mji mkuu wa Kenya, Nairobi, madereva wa teksi za kawaida wanalalamika na kupinga vikali Uber kuingia kwenye soko.

Hatari ya kuendesha teksi ya Uber nchini kenya imekuwa kubwa hadi polisi na wizara ya uchukuzi imeingilia kati.

Huku hayo yakiendelea Uber inaendelea kueneza mabawa yake baada ya kuanzisha huduma zake katika mji wa Pwani, Mombasa.

Mwandishi wetu Ferdinand Omondi ametuandalia taarifa ifuatayo.