Saratani
Huwezi kusikiliza tena

Mashine ya matibabu ya kansa Uganda yaharibika

Msemaji wa idara ya kutibu saratani katika hospitali kuu ya Mulago ameambia BBC kwamba walipokea wagonjwa elfu nne mwaka uliopita. Asilimia 75 ya wagonjwa hao walihitaji matibabu ya Radiotherapy.

Miongoni mwa magonjwa yanayotibiwa kwenye hospitali hiyo ni pamoja na saratani ya matiti, saratani ya uzazi na saratani ya tezi dume. Hospitali ya Mulago ndio taasisi kubwa zaidi ya matibabu nchini Uganda na hushughulikia magonjwa makubwa.

Wagonjwa sasa watalazimika kutafuta matibabu nje ya nchi ambayo ni ghali au kusubiri kununuliwa kwa mashine mpya ambayo inagharimu dola milioni mbili. Mashine hii aina ya Cobalt 60 hutoa miali nururishi, yaani Radioactive, kuangamiza seli za saratani katika mwili wa mgonjwa.

Ilinunuliwa mwaka wa 1995 na imekua ikiharibika mara kwa mara, licha ya kukarabatiwa. Isaac Mumena BBC Dira ya Dunia Kampala