Sokwe
Huwezi kusikiliza tena

Sokwe acheza na nyaya za umeme Japan

Sokwe mmoja aliyetoroka kutoka kituo cha kuwatunza wanyama katika mmji wa Sendai, kaskazini mwa Japan amekamatwa katika eneo la makazi baada ya kutoroka kwa saa mbili.

Sokwe huyo mwenye kimo cha mita 1.6 alitoroka kutoka kituo cha kuwatunza wanyama cha Yagiyama majira ya adhuhuri Alhamisi.

Polisi waliungana na maafisa wa kituo hicho kujaribu kumkamata mnyama huyo.

Walimfuatilia hadi alipokwea boriti ya nyaya za umeme na kisha akaanza kusonga akining’inia kwenye nyaya za umeme. Walifanikiwa kumnasa baada ya kumdunga mshale wa kumtuliza na akaanguka. Hakuna aliyejeruhiwa kwenye kisa hicho.

Kituo hicho cha wanyama kinapatikana kilomita 4 kutoka kituo cha treni cha JR Sendai na kisa hicho kilizua wasiwasi kwa muda eneo hilo.

Mkurugenzi wa kituo hicho cha kutunza wanyama Toshikatsu O-uchi aliomba radhi akisema sokwe huyo alikuwa amewekwa pahala akiwa amezuiliwa kwa nyavu lakini akazichana.

Video/Nippon Hoso Kyokai