Morogoro
Huwezi kusikiliza tena

Vijana Morogoro watumia kilimo kujifaidi

Tatizo la ukosefu wa ajira kwa vijana nchini Tanzania linazidi kuongezeka ambapo kwa mujibu wa takwimu za shirika la kazi duniani ILO zaidi ya asilimia 15 ya vijana wanakabiliwa na tatizo hilo.

Hata hivyo katika kuhakikisha wanakabiliana na ukosefu wa ajira baadhi ya vijana mkoani Morogoro Mashariki mwa nchi hiyo wamepata hamasa ya kufanya mageuzi kwenye kilimo ambapo wameamua kuanzisha kilimo cha biashara cha umwagiliaji.

Mwandishi wa BBC Esther Namuhisa alitembelea chuo kimoja cha maendeleo ya wananchi kilichopo Morogoro na kukutana na vijana wakipata mafunzo ya ukulima huo kwa vitendo.