AY
Huwezi kusikiliza tena

Sababu ya mwanamuziki AY kutotoa albamu Tanzania

Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) imeendeleza msako wa wafanyabiashara wanaouza kazi za filamu na muziki bila kubandikwa stempu halali za kodi kuzilinda kazi za wasanii.

Imesema katika kipindi kisichozidi mwezi mmoja mwaka huu, serikali imepoteza dola za Kimarekani 16,000, kutokana na kazi hizo za wasanii zilizokuwa sokoni bila ya kulipiwa kodi.

Je wasanii na wafanyabiashara wanaouza kazi za wasanii wana maoni gani kuhusu msimamo wa TRA?

Mwandishi wa BBC Tulanana Bohela alizungumza na baadhi yao akiwemo mwanamuziki AY.