Visiwani
Huwezi kusikiliza tena

Mzanzibari Mchina anayejivunia maisha visiwani

Kisiwa cha Zanzibar mbali na kuwa na vivutio vya kila aina vya Utalii, kutokana na historia yake kimejikuta pia kikikusanya watu wenye asili ya mataifa mbalimbali, kutoka Afrika, Asia mpaka Ulaya.

Wengi wazazi na mababu zao walifikafika karne au miongo kadhaa iliyopita katika harakati za kutafuta maisha ikiwemo biashara pamoja na kueneza dini.

Katika pitapita zake mjini Unguja, Mwandishi wa BBC Halima Nyanza alikutana na mmoja wa Wazanzibar hao, mwenye asili ya Uchina ambaye anajivunia kuwa Mzanzibari.