Obald
Huwezi kusikiliza tena

Padri asaidia kuponya makovu ya mauaji Rwanda

Wakati raia wa Rwanda bado wakiwa katika kumbukumbu ya miaka 22 ya mauaji ya kimbari, juhudi mbali mbali zimekuwa zikifanywa kupatanisha Wanyarwanda na kuponya makovu yaliyoachwa na mauaji hayo.

Wakati huu kuna mpango wa kipekee unaoendeshwa na padri mmoja wa Kikatoliki anayefundisha Wakristo kusameheana, wakisaidiwa na neno la Mungu.

Mpango huo umeshika kasi katika eneo la Mushaka magharibi mwa Rwanda ambako mamia ya Watutsi wameshawasamehe Wahutu walioshiriki katika mauaji ya kimbari.

Mwandishi wa BBC Yves Bucyana, alitembelea eneo hilo na kutuandalia taarifa hii.