Kiswahili
Huwezi kusikiliza tena

Lugha na utamaduni wa Waswahili ughaibuni

Matumizi ya lugha ugenini kwa kawaida hubadilika. Na hii ni changamoto hasa kwa vijana wanaokulia ughaibuni.

Vijana wanaotoka Afrika Mashariki nao wana changamoto za matumizi ya lugha ya Kiswahili ughaibuni.

Ili kutowaacha nyuma vijana hawa, baadhi ya wakazi wa London wanaozungumza Kiswahili wameanzisha mpango wa kuwasaidia vijana wasisahau lugha yao.

Ni utaratibu unaosimamiwa na kanisa la St. Anne linaloendesha ibada zake kwa lugha ya Kiswahili mjini London.

Zawadi Machibya alishiriki moja ya tamasha hizo.