Huwezi kusikiliza tena

Kenya kununua feri 2 kuimarisha uchukuzi pwani

Kwa muda mrefu, watumizi wa feri kwenye kivukio cha Likoni mjini Mombasa pwani ya Kenya wametaabika mno na msongamano.

Kutokana na idadi yao kubwa wakaazi wa Likoni hadi Vanga hulazimika kutumia feri chache za huduma ya feri ya Kenya kwa uchukuzi wao kutoka kisiwani Mombasa hadi upande wa pili wa Likoni.

Si aghalabu inapotia nanga feri huwa ni kama mkurupuko wa watu,,,, wanapojaribu kuabiri feri kila mmoja akitaka amtangulie mwenzake.

Hata hivyo nafasi kubwa huchukuliwa na magari ,iwe ni magari ya kibinafsi ama hata malori makubwa ya uchukuzi feri ni ile ile.

Lakini sasa kuna afueni.

Mwandishi wetu mjini Mombasa John Nene alipata fursa ya kuzungumza na mkurugenzi wa shirika la feri Bakari Gowa.