Huwezi kusikiliza tena

Marambuza: Nini maana yake ?

Tuangazie pwani ya Kenya.

Huko kuna neno lipya Marambuza.

Je unajua maana yake?

Kina mama mjini Mombasa wamekuwa wakilalamika kunyanyaswa kijinsia wakiwa ndani ya feri kwenye kivukio cha Likoni kinachounganisha kisiwa cha Mombasa na Kusini mwa pwani ya Kenya na hata taifa jirani la Tanzania.

Mwandishi wetu John Nene alizuru pwani ya Kenya na kuabiri feri ya MV Nyayo moja kati ya Feri 4 zinazotumika kwa uchukuzi wa mamilioni ya watu magari na mali kila siku.

Ametuandalia taarifa hii inayoelezea maana ya neno Marambuza.