Ruby
Huwezi kusikiliza tena

Ruby azungumzia safari yake kimuziki

Miaka michache iliyopita ungetaja neno Ruby nchini Tanzania wengi wangeelekeza akili zao kusini mwa nchi hiyo Mkoani Ruvuma yanakopatikana madini mekundu yaitwayo Ruby.

Lakini katika miaka ya hivi karibuni neno Ruby likitajwa kinachokuja akilini ni sauti nyororo ya Mwanadada Hellen Majeshi ambaye anatamba na vibao vyake motomoto vilivyojaa maneno ya mahaba.

Mwandishi wa BBC Arnold Kayanda amezungumza na Ruby kuhusiana na maisha yake na safari ya kimuziki na hapa Ruby anaanza kuusihi moyo wake.