Riyadh Mahrez
Huwezi kusikiliza tena

Kinyozi wa Mombasa anayewanyoa Mahrez na Kante

Jumamosi Leicester City walkabidhiwa kombe la Ligi kuu ya Uingereza baada ya timu hiyo ndogo kutwaa ubingwa kwa mara ya kwanza kabisa, wakiwapiku majogoo kama Tottenham, Manchester City na Arsenal. Wachezaji wa Leicester City wamekuwa wakitangamana na watu wa kawaida katika mji huo. Kinyozi Mmoja katika mji huo Najim Nagy anayetokea Mombasa ndiye amekuwa akiwanyoa wachezaji nyota wa Leicester Riyadh Mahrez na Ngolo Kante. Zuhura Yunus alimtembelea hapo katika kinyozi kuzungumza naye.