Uganda
Huwezi kusikiliza tena

Maktaba za pikipiki zawafaa watoto Uganda

Unawezaje kulifanya taifa likapenda kusoma vitabu? Hiyo ni kazi ngumu kwa nchi kama vile Uganda ambako bei za vitabu vya riwaya gharama yake ni sawa na ujira wa wiki nzima kwa walio wengi.

Ufumbuzi wa hili unaweza kuanzia kwa watoto. Juhudi mpya ya maktaba ya watoto inayotembea huenda ikaleta matumaini mapya na kubadili mwelekeo nchini huumo. Vitabu husafirishwa kwa pikipiki maarufu kama bodaboda.

Mwandishi wa BBC Siraj Kalyango akiwa Kampala anaeleza zaidi.