Huwezi kusikiliza tena

Mabasi ya mwendo wa kasi yazinduliwa Tanzania

Mamia ya abiria wa jiji la Dar es Salaam Jumanne walipata usafiri wa dezo na kufurahia mabasi mapya baada ya mabasi hayo kuanza kazi jijini humo.

Mradi huo unafanywa kwa ubia kati ya serikali na wamiliki binafsi wa mabasi.

Ni mfumo mpya unaotarajiwa kukabiliana na changamoto kadhaa za usafiri ikiwemo foleni na usafiri wa uhakika.

Mwandishi wetu Sammy Awami ameungana na abiria kutazama mradi huu mpya.