Besigye
Huwezi kusikiliza tena

Mke wa Besigye ajawa na wasiwasi kuhusu mumewe

Winnie Byanyima, mke wa kiongozi wa upinzani nchini Uganda Kizza Besigye, ameiambia BBC kuwa ana wasiwasi mkubwa kuhusu mumewe.

Besigye alikamatwa Jumatano baada ya kujiapisha mwenyewe kuwa rais wa Uganda katika sherehe zisizo rasmi.

Anasema uchaguzi wa mwezi Februari ulikuwa na utata. Mapema Alhamisi Yoweri Museveni aliapishwa rasmi kuwa Rais wa Uganda wa awamu ya tano.

Mwandishi wetu Siraj Kalyango alikuwepo katika sherehe hizo na kukutumia taarifa hii.