DR Congo
Huwezi kusikiliza tena

Mwanamume mzee zaidi mashariki mwa DR Congo?

Nchini Jamuhuri ya Kidemokrasia ya Congo, ni vigumu kuona watu wenye umri zaidi ya miaka mia moja na zaidi katika baadhi ya miji na vijiji.

Katika kijiji cha Ngalula kusini mwa mji wa Bukavu, mashariki mwa nchi hiyo, Mzee Petelo Sangya Shabani anaminika kuwa mkongwe zaidi eneo hilo akiwa na miaka 115.

Endapo atabahatika kuishi miaka miwili zaidi, atakuwa amemzidi umri Bi Susannah Mushatt Jones aliyekuwa mkongwe zaidi duniani na ambaye alifariki majuzi akiwa na miaka 116 New York, Marekani.

Mwandishi wa BBC Byobe Malenga alimtembelea nyumbani kwake.