Aliyekuwa waziri mkuu Kenya Raila Odinga
Huwezi kusikiliza tena

Odinga: Tume ya uchaguzi ni sharti ibadilishwe

Kiongozi wa upinzani wa Kenya, Raila Odinga ameiambia BBC kwamba hakutakuwa na uchaguzi mwakani kama maafisa wa tume ya uchaguzi hawatobadilishwa.

Waziri mkuu huyo wa zamani amekuwa akiongoza maandamano kila Jumatatu, katika mji mkuu Nairobi, kutaka maafisa wa tume hiyo kujiuzulu.

Baadhi ya maanadamano anayoongoza yamekuwa na vurugu na uporaji wa mali pia. Mwandishi wetu Anne Soy amezungumza na Bwana Odinga mwanzo akitaka kujua kama hamna njia mbadala