Mwanamuziki Ali Kiba kutoka nchini Tanzania aweka mkataba na Sony Music
Huwezi kusikiliza tena

Ali Kiba aweka kandarasi na kampuni ya Sony

Muziki wa kizazi kipya nchini Tanzania unazidi kupata nafasi ya kuwa muziki mkubwa duniani.Hii ni baada ya msanii Ali Kiba kusaini mkataba na kampuni ya Sony , kampuni inayojihusisha na kazi ya kusimamia wasanii.Baadhi ya wasanii wengine wakubwa wa kimataifa waliosimamiwa na Sony ni kama Beyonce, John Legend na Chris Brown. Mwandishi wetu Omary Mkambara amezungumza na msanii huyo na hii hapa taarifa yake.