Amanyambo
Huwezi kusikiliza tena

Wakazi Karagwe wanavyoenzi utamaduni wao

Mwishoni mwa juma dunia imeadhimisha siku ya utamaduni ulimwenguni.

Wilaya ya Karagwe inayoiunganisha Tanzania katika eneo la kaskazini magharibi na nchi za Rwanda na Uganda inasifika kwa utamaduni unaorithishwa kutoka kizazi kimoja hadi kingine kwa zaidi ya miaka 600.

Wazee wa eneo hilo lililokuwa la kifalme wameamua kuitumia wiki nzima kuikumbusha jamii juu ya utamaduni wa kale kutokana na hofu ya kuharibiwa na utandawazi.

Mwandishi wetu Arnold Kayanda amehudhuria tukio hilo na ametutumia taarifa ifuatayo.