Ruto
Huwezi kusikiliza tena

Ruto azungumzia maandamano ya upinzani Kenya

Watu watatu wameuawa na wengine kadhaa kujeruhiwa wakati polisi wa kuzuia ghasia walipokabiliana na waandamanaji wa upinzani katika miji mikubwa nchini Kenya wakitaka Tume ya Uchaguzi ijiuzulu.

Mtu mmoja amethibitishwa kufa mjini Kisumu na wawili zaidi inaripotiwa wameuawa mji jirani wa Siaya. Chama kikuu cha upinzani CORD kimetoa wito kufanyika maandamano kila Jumatatu mpaka Tume itakapojiuzulu kabla ya uchaguzi mkuu mwakani. Upinzani unaituhumu Tume kupendelea chama kilichopo madarakani.

Awali mwandishi wetu Zuhura Yunus alizungumza na Naibu Rais wa Kenya William Ruto ambaye yuko mjini Istanbul Uturuki kuhudhuria mkutano wa kimataifa kuhusu njia za kuwasaidia wakimbizi duniani, na kumuuliza kwa nini Polisi wameendelea kutumia nguvu dhidi ya waandamanaji.