Ethiopia
Huwezi kusikiliza tena

Wimbi la kuteleza kwa ubao lavuma Ethiopia

Mchezo wa kuteleza kwa ubao umeanza kuvuma nchini Ethiopia na vijana wengi wanaukumbatia mchezo huo. Hata hivyo, kuna changamoto tele.

Vijana hao wameanzisha kundi la Ethiopia Skates lakini hakuna viwanja vingi Ethiopia vya kutumiwa kwa mchezo huo.

Aidha, maduka ya vifaa na mavazi maalum ni machache mno.

Mwandishi wa BBC Hassan Lali aliwatembelea wachezaji hao na kuandaa taarifa hii.