Gambella
Huwezi kusikiliza tena

Watoto 50 waliotekwa Ethiopia wasalimishwa

BBC imepewa nafasi ya pekee kwa baadhi ya watoto hamsini na watatu ambao wameungana na familia zao hivi karibuni.

Watoto hao walikamatwa katika ghasia zilizotokea mpakani kwenye mji wa Gambella, zaidi ya mwezi mmoja uliopita.

Zaidi ya watu 200 waliuawa kwenye shambulio hilo.

Serikali ya Ethiopia imewashutumu wakuu wa kabila la Murle kutoka nchi jirani ya Sudan Kusini kwa kufanya shambulio hilo.

Harakati nyingine za kijeshi zinaendelea ili kuwaokoa watoto wengine waliochukuliwa mateka.

Emmanuel Igunza anaarifu zaidi.