Sukari
Huwezi kusikiliza tena

Mbona sukari imeadimika sana Tanzania?

Kama unapenda sukari, na unaichukulia kihivi hivi tu, ukadhani kunywa chai au kahawa yenye sukari ni jambo la kawaida, basi huna budi kuanza kuwafikiria watanzania na kizungumkuti cha sukari.

Kwa wiki kadhaa sasa imekuwa bidhaa adimu na imepanda bei. Kwa muda huu wote nchi imekumbwa na uhaba wa sukari-licha ya kuwa mzalishaji mkubwa wa bidhaa hiyo. Kwa hiyo, nini hasa kinaendelea Tanzania kuhusu sukari?

Mwandishi wetu Sammy Awami amefuatilia sakata hili.