Congo
Huwezi kusikiliza tena

Mauti yakumba maandamano DR Congo

Polisi wamefyatua risasi wakati wa makabiliano na waandamanaji huko Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo. Mmoja wa waandamanaji ameuawa huko Goma mashariki mwa nchi hiyo.

Askari mmoja wa kike amepigwa sana, huku ripoti moja ikidai kuwa kauawa. Kwenye mji mkuu Kinshasa, polisi walirusha mabomu ya machozi kwa waandamanaji waliojihami na mawe.

Maandamano haya yamesababishwa na umauzi wenye utata uliotolewa na mahakama wa kuahirisha uchaguzi mkuu wa nchi hiyo uliotarajiwa kufanyika Novemba.

Kutoka Kinshasa, Mbelechi Msoshi anatueleza zaidi