Hart
Huwezi kusikiliza tena

Bendi inayovuma kwa mashairi na uigizaji Kenya

Fani ya utunzi wa muziki unaojumuisha mashairi, uigizaji na uanamitindo imeanza kupata umaarufu mkubwa nchini Kenya.

Vijana chipikuzi kutoka mitaa ya mabanda nchini humo wamekuwa wakiwatumbuiza watu mitaani, na pia kwenye vyombo vya habari kwa muziki unaolenga kuboresha jamii, na pia kuwasaidia wasanii wenyewe kujiepusha na uhalifu.

Mwandishi wa BBC Anthony Irungu amezungumza na vijana wa bendi maarufu nchini Kenya "H_art The Band" na kutuandalia taarifa ifuatayo.